Watu takriban 19 wameuawa katika shambulizi linalodhaniwa kuwa la kulipiza kisasi katika moja ya vijiji nchini Nigeria.
Kwa mujibu wa habari,shambulizi hilo limetokea siku tatu baada ya kijana kutoka katika kabila ya Fulani aliyekuwa amepotea kukutwa amekufa katika kijiji cha Ancha
Mkuu wa polisi amesema kuwa uchunguzi zaidi unaendelea lakini mpaka sasa inaonekana dhahiri kuwa shambulizi limefanywa na wachungaji wanyama wa kabila la Fulani ,kulipiza kisasi cha kijana wa Fulani aliyekutwa kakatwa kichwa baada ya kupotea mnamo Agosti 3.
Ripoti zinaonyesha kuwa kati ya waliopoteza maisha ni watu wazima 13 huku wengine 6 wakiwa ni watoto.
Watu wengine watano wameripotiwa kujeruhiwa katika shambulizi hilo.