Senegal yatangaza baraza jipya la mawaziri

Waziri Mkuu Mohammed Dionne  siku ya Ijumaa ametangaza baraza jipya la mawaziri 39,miezi miwili baada uchaguzi wa wabunge.

Kwa mujibu wa habari,mawaziri wengi wamebadilishwa nafasi zao isipokuwa 18 tu.

Waziri wa mambo ya ndani Abdoulaye Diallo amechaguliwa kama waziri wa miundombinu.Nafasi yake imechukuliwa na Alie Ndiaye.

Waziri Mkuu anaamini bunge jipya litakidhi mahitaji ya wananchi wa Senegal.

Rais wa nchi hiyo pia anaamini kuwa bunge jipya litaleta maendeleo nchini humo.

Hata hivyo rais wa zamani  Abdoulaye Wade ambae pia ni kiongozi wa upinzani amesema kuwa kamati mpya ya bunge imechaguliwa kupendelea marafiki wa karibu wa rais mpya.
Mpya zaidi Nzee zaidi