Mamia wajitokeza kutoa heshima mwili wa aliyekuwa mke wa mkuu wa jeshi

Naibu spika Mh. Dkt Tulia Ackson ameongoza mamia ya waombolezaji waliojitokeza kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mke wa mkuu wa jeshi  la kujenga taifa Bi. Loyce Michael Isamuhyo aliyefariki dunia nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu ya kichwa.

Shughuli za kuaga mwili huyo kabla ya kusafirishwa kupelekwa mkoani Mara zilifanyika nyumbani kwake Tabata Kinyerezi jijini Dar es Salaam ambapo ibada maalum ilifanyika nyumbani hapo na kuongozwa na paroko  Evarist Tarimo kutoka  parokia ya mtakatifu Gaudence Makoka ambaye alisema kila mtu atakufa cha msingi ni kujiandaa.

Baada ya kukamilika kwa ibada hiyo mjukuu wa marehemnu Dalphine David alisoma wasifu wa maremu ambapo katika wasifu huo alisema kuwa alikuwa mwalimu na alifundisha shule mbalimbali ndani na nje ya Dar es Salaam.

Mbali na Dkt.Tulia alikuwepo Mkuu wa majeshi nchini Jenerali Venance Mabeyo, kamishina wa jenerali wa uhamiaji Dkt. Anna Makakala, mkuu wa jeshia la polisi Simon Sirro, wakuu wa vikosi balimbali vya usalama ,wabunge na makatibu wakuu
Mpya zaidi Nzee zaidi