Waziri aunda tume

Uzalishaji wa ngombe katika ranchi ya Kongwa mkoani Dodoma umepungua kiasi cha kusababisha kiwanda cha Tanzania Meat Company (TMC) cha mjini Dodoma kukosa wanyama wa kuchinja, hali iliyosababisha kushuka kwa uzalishaji na mpato ya kiwanda hicho.

Akiwa katika ziara Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, amebaini kupungua kwa uzalishaji wa ngombe katika ranchi hiyo na kushindwa kutoa gawio kwa serikali kutoka katika mapato yake. Aidha waziri Mpina ametoa maagizo kwa mkurugenzi na watendaji wote wahakikishe wanapanua uzalishaji na kuongeza idadi ya mifugo mara dufu hadi kufikia mwezi Desemba 2018.

Wakitoa maelezo ya sababu za kushuka kwa uzalishaji Meneja wa Kiwanda cha Nyama TMC Dodoma, Nashon Kalinga na Mkurugenzi na NARCO Prof Philimon Wambura kwa pamoja wamesema

Hata hivyo waziri Mpina ameunda tume ya watu watano kuchunguza sababu za kushuka kwa uzalishaji na kushindwa kupata faida kwa miaka mitano.
Mpya zaidi Nzee zaidi