https://monetag.com/?ref_id=TTIb Anusurika kifo akidaiwa kumuua mtoto wake | Muungwana BLOG

Anusurika kifo akidaiwa kumuua mtoto wake

Jeshi la Polisi Mkoani Rukwa limefanikiwa kumuokoa na kifo msichana Anastazia Elias aliyekuwa akishambuliwa na wananchi wenye hasira kali akituhumiwa kutaka kumuua mtoto wake baada ya kujifungua.

Wananchi wakiwa na silaha za jadi walianza kumshambulia mwanamke huyo wakimtuhumu kumuua mwanawe wa kiume baada ya kujifungua ambapo alimviringisha na vipande vya khanga na kumuweka kwenye kikapu alichokificha chini ya uvungu wa kitanda chake.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea juzi saa nane mchana katika Kijiji cha Kipundu kilichopo mjini Namanyere.

Kamanda Kyando amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Polisi wilaya Nkasi na kwamba atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi wa tukio kukamilika.

Wakizungumza baadhi ya wanawake  wamedai mtoto huyo alizikwa juzi usiku katika kaburi lililochimbwa ndani ya nyumba ambayo mama yake mzazi anaishi na bibi yake.

Akisimulia tukio hilo, Diwani wa Kata ya Kipundu, John Kapandila alisema mchana wa siku ya tukio, watoto wadogo walimuona mwanamke huyo akiwa amebeba kitu kwenye mfuko wa plastiki na kwenda chooni alipotoka hakurudi nao. “Watoto hao walikimbia na kuwataarifu wazazi wao kuwa Mama Baraka amejifungua mtoto, lakini amemtupa chooni.