Aubameyang awafungukia wanaomfuatilia maisha yake

Supastaa wa klabu ya Arsenal na Timu ya Taifa ya Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang amegoma kupangiwa namna ya kuishi huku akisisitiza kuwa, kamwe hawezi kubadili mtindo wake wa maisha eti kisa tu watu hawapendezwi nao.

Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Gabon amelazimika kuweka wazi hilo baada ya kuulizwa na mwandishi kuwa aina yake ya maisha ikiwemo kuendesha gari kwa kasi na kunyoa mitindo mbalimbali imekuwa ikijadiliwa sana lakini Aubameyang amesisitiza kuwa hiyo ndio furaha yake.

"Ninapenda kufanya vitu vinavyonitambulisha kuwa mimi ni nani na haijalishi kama watu wengine hawawezi kukubaliana na mimi'', amesema.

Aubameyang amesisitiza kuwa akiwa uwanjani anapenda kufanya vitu ambavyo vitawafurahisha mashabiki wake kama kufunga mabao mengi iwezekanvyo lakini lnapokuja suala la kuishi ndoto zake za utotoni hapendi kupangiwa na mtu yeyote.
Mpya zaidi Nzee zaidi