Popo wamevamia Zahanati ya Kiria iliyopo Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro na kuharibu majengo, hali ambayo imezua taharuki kwa wagonjwa wanaofika kupata huduma za matibabu.
Popo hao wanaotajwa kuwa zaidi ya 1,000 wameharibu dari la zahanati hiyo na kusababisha harufu kali katika wodi za wagonjwa, ikiwemo ya wajawazito ambayo milango yake imeegeshwa kwa mawe kutokana na kutafunwa na mchwa.
Mjumbe wa kamati ya maendeleo wa zahanati hiyo, Bakari Karani amesema leo Februari 15, 2018 kuwa hali ya zahanati hiyo imekuwa kero kwa muda mrefu.
“Milango imeliwa na mchwa, popo zaidi ya 1,000 wamevamia maeneo yote ya zahanati na kuleta kero kubwa kwa wagonjwa na wahudumu nyakati za usiku na mchana,” amesema.
Ameiomba halmashauri ya wilaya hiyo kupambana na mchwa na popo hao ikiwa ni pamoja na kukarabati majengo hayo ili wagonjwa waweze kupata huduma za afya katika mazingira safi na salama.
“Popo wamekuwa ni tishio kubwa na hatari kwa wagonjwa kwani wagonjwa wanapolazwa wanashindwa kupata hewa safi kutokana na uharibifu wa popo hawa,” amesema.
Muuguzi wa zahanati hiyo, Helena Shaban amesema inakabiliwa na uchakavu wa majengo pamoja na upungufu wa wahudumu wa afya, hususan panapotokea magonjwa ya milipuko kama kipindupindu.
“Kijiji chetu kina magonjwa ya milipuko kama kipindupindu, hivyo tunashindwa kuwahudumia wagonjwa kwa wakati. Kwa kweli mazingira ya hapa ni magumu na tunafanya kazi katika mazingira hatarishi,” amesema.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Golden Mgonzo amesema ofisi yake haikuwa na taarifa ya uharibifu wa majengo ya zahanati hiyo na kuahidi kufanya ukarabati kuanzia Februari 19, 2018.
“Ofisi yangu imepokea kero hiyo na naahidi kulifanyia kazi na nitaanza chumba cha upasuaji na dari za wodi za kupumzishia wagonjwa kwa sababu zahanati hii imejengwa toka mwaka 1981 na ramani yake ni ya zamani,” amesema.
Amesema fedha za ukarabati huo zitatoka katika mapato ya ndani ya makusanyo ya halmashauri hiyo, na kwamba wamejipanga kujenga jengo la kisasa katika zahanati hiyo kwa ajili ya kutolea huduma za afya.