Rais wa klabu ya Paris St. Germain ya Ufaransa, Nasser Al-Khelaifi amelionya shirikisho la mpira barani Ulaya (UEFA) kujitafakari na kuchunguza namna ya waamuzi wao wanavyochezesha mechi zao hususani pale timu za Hispania zinapocheza kwenye michuano mikubwa barani humo.
Al-Khelaifi amesema hayo jana mbele ya waandishi wa habari baada ya timu yake kupoteza mchezo wa kwanza wa klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Real Madrid kwa goli 3-1.
“Mwaka jana tulipoteza mchezo na Barcelona katika mazingira ambayo huwezi kutazamia, mwaka huu tena tunafungwa na Real Madrid kwa maamuzi mabovu ya waamuzi, Nadhani kuna jambo UEFA wanapaswa kujitafakari hususani timu za Hispania zinapocheza michuano mikubwa, Tumekuwa wahanga wa kufungwa yaani marefa wamekuwa kwenye matangazo ya timu za La Liga,“amesema Al-Khelaifi.
Hayo yamejiri baada mshambuliaji wa Real Madrid, Toni Kroos kwenye mchezo huo wa jana kuangushwa kwenye eneo hatari la PSG kitu kilichopelekea Refa kutoa maamuzi ya penati iliyozua utata.
Mwaka jana March 8 kwenye marudiano ya mchezo wa 16 Bora kati ya Barcelona na PSG, Barcelona waliichabanga PSG goli 6-1 na kuwatupa nje ya michuano hiyo.
