Rais wa Ufaransa na Rihanna wapongeza sekta ya elimu barani Afrika

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron  amefahamisha kuongeza juhudi na ufadhili  katika mpango wa elimu kwa thamani ya karibu dola milioni 250 kinyume na ilivyokuwa katika kipindi cha kati ya mwaka 2014 na mwaka 2017.

Jumuiya ya kimataifa  katika mkutano wake uliandaliwa mjini Dakar Ijumaa kupiga atua na kutoa msaada katika zoezi la kuimarisha sekta ya elimu kwa watoto ikiwemo barani Afrika .

Atua hiyo imepongezwa na kuungwa mkono na nyota wa muziki wa kimataifa Rihanna.

Ushirikiano wa kimataifa wa elimu upo katika  muelekeo mzuri jambo ambalo  linaitaji  kuongezwa kiwango cha dola bilioni 3,1. Haya ni baada ya mkutano uliofanyika mjini Dakar chini ya uongozi wa rais Maky Sall na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron  katika izra yake rasmi nchini Seengal.

Mkutano huo uliwajumuisha  viongozi tofauti wa bara la Afrika na  wawakilishi wa mashirika ya kutoa misaada.

Mkutano huo  umeonesha kutoa kipaumbele kupunguza idadi ya watoto wasiokwenda shuele katika mataifa ambayo yamekumbwa na umaskini.

Ufaransa imetoa mfano kwa kuongeza kiwango chake katika zoezi hilo ikifuatiwa na Uingereza  kwa kutoa kiwango cha dola  milioni 417, Umoja wa Ulaya dola milioni 400 na Norway dola milioni 260.
Mpya zaidi Nzee zaidi