Zimbabwe yahimizwa kuendeleza mageuzi ya sera ya ardhi

Uingereza imeitaka Zimbabwe kuendelea na hatua ya uwazi na usawa katika suala la mageuzi ya ardhi.Hayo yamezungumzwa na waziri anayehusika na masuala ya Afrika wa Uingereza Harriet Badwin baada ya kuwa na mazungumzo na rais Mnangagwa mjini Harare kuhusiana na suala hilo la ardhi.

Utawala mpya wa mjini Harare umekuwa ukijaribu kuleta mageuzi katika sera ambazo zilisababisha maelfu ya wakulima wakizungu kufukuzwa katika mashamba yao nchini Zimbabwe bila ya kulipwa fidia.

Rais Mnangagwa kwa sasa anafanya juhudi za kuimarisha uchumi pamoja na kurekebisha mahusiano na nchi ambazo ziliiwekea vikwazo nchi yake chini ya utawala wa mtangulizi wake Robert Mugabe.
Mpya zaidi Nzee zaidi