" Nimeshazoea maisha ya huku, sipati changamoto tena" Msuva

Winga wa timu ya taifa ya Tanzania na Klabu ya Difaa El Jadidda ya Morocco Simon Msuva, amesema kwasasa amezoea mazingira na maisha ya Morocco baada ya mwanzo kupata changamoto ya lugha pamoja na aina ya vyakula.

Msuva amesema hayo kwenye mahojiano kwa njia ya simu na East Africa Television ambapo ameeleza uzoefu wake kwasasa katika maisha ya kawaida na ya uwanjani nchini Morocco ambapo yupo kwenye msimu wake wa kwanza.

''Namshukuru Mungu naendelea vizuri, zile changamoto nilizokuwa nakutana nazo zimeisha, kwamfano vitu kama lugha, japo lugha ya mpira ni moja hivyo nimezoea lakini pia vyakula na aina ya soka ya hapa pamoja na waaamuzi'', amesema Msuva.

Kwa upande mwingine Msuva amewashauri wachezaji wa Tanzania kuwa na utamaduni wa kujaribu soka la kimataifa kwani wanauwezo mkubwa na watafanikiwa kama ilivyo kwake.
Mpya zaidi Nzee zaidi