Pierre-Emerick Aubameyang akishangilia baada ya kuifungia Arsenal mabao mawili dakika za 75 kwa penalti na 86 katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Stoke City kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates, London. Bao lingine la Arsenal limefungwa na Alexandre Lacazette kwa penalti pia dakika ya 89.
