Wanajeshi watatu wa Saudi Arabia wauawa mpakani mwa Saudi Arabia na Yeman

Taarifa zilizotolewa na kituo cha habari cha Saudi Arabia SPA zimefahamisha kuwa wanajeshi watatu wameuawa katika eneo la mpakani mwa Saudi Arabia na Yemen. Wanajeshi hoa wameuawa  wakiwa katika wajibu wao wa kutumikia taifa katika eneo la Jazan.

Taarifa kuhusu kilichopelekea wanajeshi hao kufariki hazijafahamishwa.

Saudi Arabia inaongoza jeshi la ushirika katika operesheni ya kijeshi ilioanzishwa Yemen dhidi ya wanamgambo wa Houthis.
Mpya zaidi Nzee zaidi