4/16/2018

Ruvu Shooting yaipiga Ndanda FC 3-1

Kikosi cha Ruvu Shooting kimezidi kuamka kunako ligi kuu kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ndanda FC uliopigwa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Ruvu wamejipatia mabao hayo kupitia kwa Baraka Mtuwi (24'), Adam Ibrahim (40') na Fully Maganga (45').

Bao pekee la kufutia machozi kwa Ndanda limefungwa na Omary Mponda katika dakika ya pili tu ya mchezo.

Mbali na Ruvu Shooting kupata matokeo hayo, huko Kaitaba Kagera Sugar imeweza kuanza kujikwamua kushuka daraja baada ya kuifunga Mtibwa kwa mabao 2-1.

Mabao hayo yamefungwa na Japhary Kibaya kwenye dakika za 45 na 53+', Mtibwa walipata goli kupitia kwa Salum Kihimbwa (26').