https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mwanafunzi auawa kikatili | Muungwana BLOG

Mwanafunzi auawa kikatili

Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Old Tanga, Shufaa Mbughuni amekutwa amefariki dunia huku uso wake ukiwa umechubuliwa ngozi.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tanga, Edward Bukombe amesema mwili wa mwanafunzi huyo umekutwa jana Agosti 19, 2018 saa 9.40 alasiri katika mtaa wa Majani Mapana kata ya Nguvumali jijini Tanga.

Bukombe alisema taarifa kamili kuhusiana na tukio hilo ataitoa  mara baada ya madaktari wa hospitali ya mkoa wa Tanga ya Bombo kuufanyia uchunguzi mwili wa mwanafunzi huyo.

Naye baba wa mwanafunzi huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Majani Mapana, Salim Mbughuni amesema mwanaye aliwaaga wenzake juzi saa 2.00 usiku kwamba anakwenda kijisomea lakini hakurudi kama ilivyo kawaida yake.