Hii kali, Wauguzi 16 wa Hospitali moja wabeba mimba kwa pamoja

Wauguzi hao wakiwa katika picha ya pamoja.

Asilimia 10 ya wahudumu wa chumba cha uangalizi maalum ( ICU), wameanza kugundua ongezeko la wingi wa wauguzi kuwa wajawazito, ambapo wauguzi 16 wana ujauzito kwa wakati mmoja katika hospitali ya Mesa,Arizona huko nchini Marekani.

Katika mkutano na wanahabari, ,wanawake hao walitania kuwa lazima kutakuwa na kitu kilichosababisha hali hiyo au labda walikuwa mapumziko ya sherehe za Krismasi pamoja, mwaka jana.

Katika kundi hilo la wauguzi wajawazito ,wa kwanza anatarajiwa kujifungua mwezi Septemba na wa mwisho mwezi Januari 2019.

Rochelle Sherman ambaye ana mwezi mmoja tu kabla ya kujifungua amesema hawakuwa wamegundua kuwa ni wajawazito wangapi mpaka walipoanzisha kikundi katika mtandao wa kijamii wa Facebook.

"Inavyoonekana ni kama tulikuwa tumekubaliana lakini imetokea tu", amesema Rochelle.

Hata hivyo wamewashukuru wafanyakazi wenzao kuingia kwenye idara yao na kuanza kuwasaidia kazi ambazo wanawake wajawazito hawawezi kuzifanya kama vile kumhudumia mgonjwa mwenye ugonjwa wa kuambukiza kama kifua kikuu na kuwahudumia wagonjwa wa saratani.

Wafanyakazi hao watafanya sherehe ya pamoja ya kukaribisha watoto wao 'babyshower' wiki ijayo kabla hawajaenda kwenye mapumziko ya uzazi.