Rais Magufuli akutana na Mjukuu wa Malkia Elizabeth, amuhakikishia ushirikiano


Rais Dk John Magufuli leo Septemba 27 amekutana na kufanya mazungumzo na Mjukuu wa Malkia Elizabeth II wa Uingereza, Prince William ikulu jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo Prince William ameeleza kufurahishwa na uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi hizo mbili na kumshukuru Rais Magufuli kwa kupata nafasi ya kuzungumza nae.

Kwa upande wake Rais Magufuli amemkaribisha Prince William kuja nchini wakati wowote na kumhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano wake Uingereza katika kukabiliana na vitendo vya ujangili hasa wa Tembo.




Mpya zaidi Nzee zaidi