Alhamdulillah leo nimetimiza miaka kadha, HAPPY BIRTHDAY TO ME

Leo Octoba 15 ni siku yangu ya kuzaliwa hivyo napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Allah kuwa mzima na kufikisha miaka kadhaa tangu kuzaliwa kwangu.

Nifaraja kubwa sana kwangu kuiona siku yangu ya kuzaliwa pia kuweza kufika tena siku hii muhimu ya leo.

Siku hii ya leo ni siku kubwa sana kwangu napenda kuwashukuru wazazi wangu japo Baba ametangulia mbele ya haki Mungu amrehemu na amfungulie milango ya pepo Amin, Na pia napenda kumshukuru sana mama yangu ambaye siku kama ya leo aliteseka kwajili ya kunileta duniani.

Pia napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa ndugu jamaa na marafiki bila kusahau  timu nzima ya wafanyakazi wa Muungwana Blog / TV na watumiaji pia wadau wa Muungwana Blog /TV ambao wapo bega kwa bega na mimi katika kuhakikisha tulisongesha gurudumu hili la maendeleo, kwa pamoja mungu atulinde na atusimamie tuendelee kuwa na afya njema.


Mpya zaidi Nzee zaidi