10/11/2018

Mwili wa Pancho Latino Kuagwa Kesho Dar

Mwili wa  mtayarishaji huyo wa muziki Joshua Magawa maarufu kama Pancho Latino utaagwa kesho katika hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kupelekwa Gairo mkoani Morogoro kwa mazishi.

Msemaji mkuu wa shughuli hiyo ya mazishi msanii Fid Q amesema kuwa shughuli za kuaga zitaanza saa 4:00 asubuhi na baada ya hapo utasafirishwa kwao gairo ambapo wanatarajia kufika usiku.

Pancho alifariki juzi katika visiwa vya mbudya alikokuwa akiogelea