.

1/11/2019

AliKiba ni shabiki yangu mkubwa sana - Kayumba


Msanii wa Bongo Fleva, Kayumba amesema kuwa AliKiba ni shabiki yake mkubwa sana.

Kayumba amesema kuwa hajawahi kufikiria kuwa kama  msanii huyo anaweza akawa anafuatilia kazi zake.

"AliKiba ni shabiki yangu mkubwa sana anapenda sana nyimbo zangu, sikuwahi kufikiria hilo lakini nimekuja kufuatilia kuwa ni shabiki yangu mkubwa na anafuatilia sana muziki wangu," amesema Kayumba.