1/11/2019

KMC yamfunga mdomo Masau Bwire

Timu ya KMC leo imefanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa mzunguko wa 21 wa Ligi Kuu Bara, uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Bao la KMC lilifungwa na Cliff Buyoya dakika ya 66 na kuwafanya waweze kufanikiwa kucheza michezo minne bila kupoteza baada ya kuanza na sare dhidi ya Mbao, kisha ushindi mbele ya African Lyon, JKT Tanzania na leo Ruvu Shooting.

Kabla ya mpira kuanza tambo za wasemaji zilitawala kati ya Anwari Binde wa KMC 'wanaKino' na Masau Bwire wa Ruvu Shooting mzee wa kupapasa ila baada ya dakika 90 KMC waliibuka kifua mbele.

Matokeo mengine kwa mechi zilizochezwa leo ligi kuu ni ushindi wa Singida United kwa kushinda mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC huku ule dhidi ya Lipuli na JKT ukipelekwa mbele.