Msanii wa Vichekesho, Anko Zumo aliyejipatia umaarufu kwa kuigiza na mtoto wake, Maisara Zumo amesema mtoto huyo aling'ang'ania kuigiza.
Anko Zumo amesema kuwa walikuwa hawafikirii kama Mai Zumo atakuwa muigizaji hata siku moja.
"Tulikuwa hatufikiriii kama Mai Zumo atakuwa mwigizaji siku moja naye alitaka kuonekana kwenye video tukamwambia atoke asilete fujo hadi tukashindwa kufanya shughuli yetu alikuwa analia tukamwabia afanye tulilomwambia akaweza vizuri tangu siku hiyo tukaanza kumtumia,’’ alisema Anko Zumo kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.
