Polisi nchini Sudan imebaini kuwa, watu 16 wameuawa huku wengine zaidi ya 20 wakijeruhiwa katika maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.
Hayo yamesemwa Msemaji wa Polisi, Hashem Ali ambaye ameongeza kuwa, waandamanaji hao wameuawa kwa risasi na kwamba majengo ya serikali na ya kibinafsi pia yameshambulia na kuharibiwa katika maandamano hayo.
Mamia ya maelfu ya wananchi wa Sudan walimiminika katika barabara za Khartoum, katika maandamano ya kumtaka Jenerali Awad Mohamed Ahmad Ibn Auf, Waziri wa Ulinzi wa Sudan aliyetangazwa kuwa Kaimu Rais baada ya Omar al-Bashir kung'olewa madarakani ajiuzulu.
Tayari Jenerali Ibn Auf ametangaza kujiuzulu, huku akimteua Luteni Jenerali Abdel Fattah Burhan, Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Nchi Kavu kujaza nafasi yake.
