Dk. Tizeba akili uvuvi haramu tishio


Na. James Timber, Mwanza

Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Dk. Charles Tizeba ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Kilimo mifugo na uvuvi pia Waziri wa kilimo amekili wazi kuwa uvuvi haramu bado ni tishio Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema.

Kauli hiyo ameitoa jana mbele ya Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi, Abdallah Ulega wakati wa uzinduzi wa soko la kimataifa la kukununua na kusafilisha samaki lililoko Kata ya Nyakalilo Halmashauri ya Buchosa.

Soko hilo lilianza kujengwa mwaka 2012 limegharimu kiasi cha shilimgi milioni 223, soko hilo lilijengwa kwa ufadhili wa kutoka nchi ya Japani.

Akitoa salamu  za jimbo hilo kwa naibu waziri wa mifugo na Uvuvi Tizeba alisema anaishukuru serikali kwa kusikia kilio cha wadau wa uvuvi jimbo la Buchosa na Wilaya ya Sengerema kwa ujumla kwa kufungua soko la samaki la Nyakalilo kuwa soko la kimataifa na litafungua furusa za kibiashara kwa wafanyabiashara wa sengerema na matafia ya nje na kukuza uchumi wao.

Halmashauri ya Buchosa ni miongoni mwa Halmashauri nane zinazounda mkoa wa mwanza ina tarafa 2 Kata 21 vijiji 82 na vitongoji 410 inaidadi ya wakazi 327,767 kwa mjibu wa sense ya mwaka2012  , makadilio ya mwaka 2017 ni watu 390.588 kwa ongezeko la asilimia 3.6.

Licha ya kufungua soko hilo Tizeba aliitaka Wizara ya Mifungo na uvuvi kuongeza jitihada za kupambana na uvuvi haramu ambao bado ni tishio Halmashauri ya Buchosa ili kuokoa maisha la samaki wachanga ambao bado wanateketea.

"Uvuvu haramu bado upo na leo ungekuja kimya kimya ungejionea wazi ,watendaji wa wizara yako bado hawajaelewa mheshimiwa Rais anataka nini wekeni kambi huku dhibitini uvuvu haramu," alisema Tizeba.

Kauli ya Tizeba ilimchanganya Naibu Waziri wa uvuvi Abdallah Ulega  wakati akifungua soko la samaki la kimataifa la Nyakalilo na kutoa onyo kali kwa maafisa uvuvi kufanya kazi  wazizosomea na kuangizwa na serikali ili kuzitekeleza.

Ulega aliwataka maafisa uvuvi kujitathimini juu ya utendaji wao wa kazi kutokana na vitendo vya uvuvi haramu kuendelea katika maeneo yao na kuwataka warekebike la sivyo watakutana na mfagio wa chuma.

"Serikali inatumia fedha nyingi kupambana na uvuvi haramu, kunabadhi yenu siyo waaminifu  wanachukuwa rushwa na uvuvi haramu unaendelea tukiwabaini tuwachulia hatua za kinidhamu," alisema Ulega.

Akisoma taarifa ya soko la samaki la Nyakalilo mbele ya Naibu Waziri wa mifungo na uvuvi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa Crispin Luanda alisema sekta ya uvuvi ni miongoni mwa shughuli za uchumi zinazofanywa katika Halmashauri ya Buchosa na sekta hiyo inachangia asilimia 71 ya makusanyo ya mapato ya halmashauri hiyo na asilimia 29 zinatoka kwenye vyanzo  vingine.

Luanda alisema katika kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2016/17 , 2017/18 na hadi Mei 2019 makusanyo kutoka sekta ya uvuvi yameifika shilingi bilioni 4.

"Makusanyo hayo yanatokana na leseni za vyombo vya  uvuvi, leseni za uvuvi pamoja na ushuru wa samaki hivyo kufunguliwa kwa soko hili la Nyakalilo kutaongeza mapato makubwa kwenye Halmashauri," alisema  Luanda.

Afisa Mifugo na uvuvi wa Halmashauri ya Buchosa Shija Lyela alisema kuwa Halmashauri hiyo ina mitumbwi 6461, mitumbwi ya kasia 2,107 na mitumbi ya injini 4,354 na wavuvi wapatao 19,383.

Lyela alisema jitihada mbalimbali zinachuliwa na Halmashauri ya Buchosa dhidi ya uvuvi haramu ,jitihada hizo ni pamoja na ununuzi wa boti 1 kwa ajili ya doria za mara kwa mara na kutoa elimu kwa wadau wa uvuvi juu ya uvuvi endelevu.

Mmoja wa wananchi Halmashauri ya Buchosa Juma Lutanda alisema vitendo vya uvuvi haramu haviwezi kuisha hadi wafanye mabadiliko ya kuwahamisha maafisa uvuvi.
Mpya zaidi Nzee zaidi