Mfungwa anayetajwa kuwa mzee zaidi nchini Nigeria mwenye umri wa miaka 100 aliyekuwa anatumikia kifungo cha maisha jela amesamehewa.
Celestine Egbunuche ameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupokea msamaha wa jimbo la Enugu.
Yeye na mwanaye wameshatumikia kifungo cha miaka 18 gerezani kwa kosa la kupanga njama ya mauaji. Hata hivyo mwanaye amesalia gerezani kuendelea kutumikia kifungo chake.
