Mambo matano atakayofanya Diamond Platnumz Mwaka huu


Msanii wa Muziki, Diamond Platnumz ametaja mambo makubwa ambayo atavifanya mwaka huu.

Diamond amesema kuwa kutakuwa na sherehe ya miaka 10 ya Diamond Platnumz, kutakuwa na Wasafi Festival na baadhi ya birthday.

"Mwaka huu tunavitu vingi kumbuka tutakuwa na sherehe ya miaka 10 ya Diamond Platnumz, kutakuwa na Birthday kubwa itafanyika ya kwangu, kuna Birthday ya mama, ya mpenzi wangu alafu tuna Wasafi Festival ambayo inaanza mwisho wa Mwezi huu mkoa kwa mkoa," alisema Diamond Platnumz akiwa Geita.