CECAFA yawajibu Simba SC na Yanga SC baada ya kususia Kagame CUP


Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye amesema mashindano ya Kagame Cup 2019 yataendelea licha ya kutokuwapo Simba na Yanga. Amesema Yanga ni timu isiyo na msaada, ndio sababu hufungwa 5-0 au 6-0 kwenye mashindano ya kimataifa. Mashindano hayo ya timu 16 yatafanyika Julai 17-21.

Utakumbuka hapo jana Klabu ya Yanga imesema haitoshiriki michuano ya Kagame Cup yatakayofanyika mwezi Julai 2019, jijini Kigali, Rwanda kwa sababu, wachezaji wengi wamemaliza mikataba, wengine wapo na timu ya taifa, na waliobaki wapo mapumziko.

Wakati hayo yakijiri, tayari Simba SC ilishatangaza kuwa haitoshiriki mashindano hayo, uamuzi huo umetokana na ratiba ya mashindano hayo kuingiliana na ratiba ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi ya Bingwa AFRIA (CAFCL) na Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL) 2019/2020.