Baada ya mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC kutangaza kujiondoa kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati Cecafa Kagame Cup 2019, watani wao wa jadi Yanga nao wamekataa mwaliko waliopewa kushiriki michuano hiyo itakayofanyika mwezi Julai nchini Rwanda.