Na Rahel Nyabal, Tabora
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amewahakikishia masoko wakulima wa Pamba.
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amekagua soko la pamba katika wilaya za Nzega na igunga huko mkoani Tabora soko ambalo limekuwa likisuasua kutokana na wanunuzi kukosa fedha za kununua zao hilo huku akiwahakikishia wakulima wa zao hili kupata fedha zao.
Mpaka sasa Wilaya za Nzega na Igunga imeelezwa kuwa zina zaidi ya kilo Milioni 30 za pamba huku ikiwa bado kilo Milioni 27 hazijanunuliwa ambapo Naibu Waziri Bashe akalazimika kutoa msimamo wa serikali kwa wakulima wote wa zao hilo hapa nchini ambao pamba yao bado haijanunuliwa.
Akiwa katika ukaguzi huo wa soko la pamba ambao umekwenda sambamba na kukutana na wakulima wa zao hilo kama alivyoagizwa na Rais John Pombe Magufuli wakati akiapishwa Ikulu jijini Dar-es-salaam Naibu waziri wa kilimo Hussein Bashe amekutana na Wakulima wa zao hilo ili kuendana na kasi ya serikari ya awamu ya Tano.
Hata hivyo katika ziara hiyo Naibu waziri Bashe amebaini mapungufu kadhaa ikiwemo Mchezo mchafu kwenye mikopo ya Pembejeo inayotolewa na vyama vya ushirika kwa wakulima wa zao pamba wamekuwa wakiibiwa.
