Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amezionya nchi za nje kutoupalilia mzozo unaohusu Bahari ya Kusini mwa China.
Hivi karibuni shughuli za China katika bahari hiyo yenye utajiri wa nishati ulizipa wasiwasi nchi nyingi katika kanda hiyo pamoja na Marekani kuikosoa China.
Wang, ambaye anatarajiwa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo huko mjini Bangkok, amesema baada ya kukutana na mawaziri wenzake wa mataifa ya jumuiya ya ASEAN kwamba China inapinga uingiliaji kati wa nchi ambazo ziko nje ya kanda hiyo.
Hivi karibuni China imesema ukosoaji wa Marekani dhidi yake kuhusu Bahari ya Kusini mwa China uliotolewa na Pompeo ni wa kashfa.