Kundi la kigaidi la Boko Haram la nchini Nigeria latumia Drone katika shughuli zake dhidi ya oparesheni za kijeshi.
Gavana wa jimbo la borno Babagana Zulum, amewaambia waandishi wa habari kwamba wanamgambo wa Boko Haram wanatumia Drone katika kuchunguza oparesheni za kijeshi, hilo linaonyesha kwamba kundi hilo la kigaidi lina teknolojia ya kisasa zaidi kuliko jeshi la nchi.
Zulum alisema pia kwamba wanamgmbo wa Boko Haram wanatumia silaha za kisasa zaidi ukilinganisha na zile zinazotumia na jeshi.
