Benki ya Dunia - Afrika yaihakikishia Serikali mkopo wa Dola BilioniI1.7

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Anne Kabagambe anayesimamia nchi 22 ameihakikishia Tanzania kuwa benki hiyo iko tayari kutoa kwa Serikali fedha zote za mkopo wa masharti nafuu kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.7 zilizobaki katika mgao wa 18 wa IDA.


Kabagambe ambaye yuko nchini kwa ziara ya kikazi amesema hayo wakati wa mazungumzo kati yake na Waziri wa Fedha, Dkt. Philip Mpango, yaliyofanyika Jijini Dar es salaam.

”Fedha hizi zitaelekezwa katika kutekeleza miradi kadhaa muhimu ikiwemo ya Elimu, Afya, Mradi wa kusaidia kaya masikini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF, Awamu ya Pili na Uendelezaji wa Miji na Masuala ya Uchumi Jumuishi Visiwani Zanzibar,” alisema  Kabagambe.


Mpya zaidi Nzee zaidi