Loading...

Aug 2, 2019

Jambo muhimu la kuzingatia katika safari yako ya mafanikio

Neno maisha ni mkusanyiko wa vipande vidogodogo ambavyo vimetawanyika na pindi vikusanywapo kwa pamoja hutengeneza kitu kinachoitwa mafanikio. Pia mafanikio hayo yameganyika katika makundi matatu, mafanikio ya juu, kati na chini.

Na moja ya sababu kubwa ya wengi wetu kushindwa kufikia kilele cha mafanikio hayo ni kwamba tumeshindwa mbinu madhubuti ya kukusanya vipande hivyo na kuviweka pamoja  ili tuweze kufankiwa.

Leo nitakueleza kipande ambacho ni muhimu  unachopaswa kukiunganisha katika maisha yako  ili uweze kufanikiwa kiurahisi, Kwani wengi wa watu ambao wameweza kufanikiwa katika sayari hii ni kwamba waliweza kufanikiwa kukiunganisha kipande hicho hatimaye kuweza kufanikiwa.

Kipande hicho si kingine bali  ni, unahitaji mtandao wa watu ili uweze kufanikiwa. Moja kati ya changamoto kubwa ambayo ipo na inaendelea kutuua taratibu ni kwamba hatuna watu sahihi ambao wanasababisha sisi kuweza kusonga mbele katika harakati za kufanikiwa.

Wengi wetu, Watu tulionao ni wale wale wa siku zote ambao ukiwambia unataka kufanya jambo fulani lenye tija ni lazima watu hao watakuleleta sababu za kushindwa tu. Watu wa aina hii hawafai hata chembe na vyema kuwaepuka mapema katika maisha pindi uwatambuapo.

Ila ukweli ni kwamba watu sahihi na wenye malengo na mitizamo chanya ndio wanaotakiwa kuyazunguka maisha yako ya kila siku iwe ni kwa kupenda au kwa kutokupenda.

Hebu fanya zoezi dogo shika simu yako kisha pekua majina ya watu mbalimbali waliopo katika simu yako, je majina mangapi yana manufaa/msaada  kwako? Jibu baki nalo.

Nimekuuliza swali hili kwa sababu asilimia 99.99 wengi wetu simu zetu zimejaa majina ambayo hayana chachu yeyote katika kuhakikisha tunapiga hatu za kimafankio. Majina mengi ya watu tuliona yanaongeza uzito wa simu tu, hapa nimeweka chumvi kidogo ila huo ndiyo ukweli halisi.

Nini kifanyike; Ukiona simu yako haina majina matano ambayo yanachangia kitu chochote kwenye maisha yako basi simu hiyo iweke kwenye maji, au izime kisha utoe betri kwani haina umuhimu wowote kwako.

Ila ukweli ni huu, Unachotakiwa kufanya ni kwamba katika maisha yako ya kila siku hakikisha ya kwamba unazungukwa na watu chanya wenye kuchangia jambo fulani katika maishha yako ya kila siku. Kama ni marafiki basi chagua marafiki ambao  mtashauriana mambo chanya na yenye kuleta tija katika maisha yako na si vinginevyo. Pia watalamu wa mambo wanasema kila wakati jifunze kuchagua marafiki ambao wamekuzidi umri.

NUKUU YA LEO; 
Mtandao wa mafanikio wenye watu chanya, ni  njia ya kufikia kilele cha mafanikio yako.

Mpaka kufikia hapo sina la ziada nikutakie siku njema na utume mwema, endelea kutembelea Muungwana blog kila wakati.
Na: Benson chonya

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger