https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mtuhumiwa ujambazi afariki akipatiwa matibabu | Muungwana BLOG

Mtuhumiwa ujambazi afariki akipatiwa matibabu


Na Timothy Itembe Mara

Mkazi wa kijiji cha Kitenga wilayani Tarime mkoani Mara,Mwita Marwa Magori kwa jina maarufu Otieno 45 ambaye alikuwa anatafutwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za makosa  ya uporaji wa mifugo amefariki Dunia mda mfupi baada ya kukamatiwa Shinyanga na kuletwa Tarime kwaajili ya maohijiano.

Kamanda Mkoa wa Kipolisi Tarime na Rorya, Henry Mwaibambe amewaambia waandishi wa habari leo Ofisini kwake kuwa Marehemu alikamatiwa mkoani Shinyanga na aliletwa Tariume kwa mahojiano zaidi juu ya tuhuma zilizikuwa zinamkabili za makosa ya Uporaji wa mifugo hususani maeneo ya Rorya Tarime  na Kahama na alikuwa na mtandao mrefu.

Marehemu katika mahojiano na askari Polisi alitupatia ushirikiano wa kutosha wa mtandao wake wa wizi wa mifugo na ujambazi ambao tunaufanyia kazi aliongeza kusema  Mwaibambe.

"Kwa mda mrefu Jeshi la Polisi lilikuwa linamtafuta Mtu aitwaye Mwita Marwa Magori maarufu kwa jina la Otieno 45 mkazi wa kijiji cha Kitenga kwa makosa ya uporaji wa mifugo ambapo alikamatiwa mkoani Shinyanga na kuletwa kwetu kwaajili ya mahojiano  gafla akiwa katika mahojiano  aliugua tumbo la kuhara na kupelekwa hospitali ya Wilaya ambapo alifariki Dunia"alisema mwaibambe

Mwaibambe aliongeza kuwa marehemu amefariki Dunia Juzi Agosi,11,2019 katika hospitali ya Wilaya inayomilikiwa na halmashauri ya Mji wa Tarime wakati akiwa anapatiwa matibabu.

Jeshi la polisi limetoa nafasi kwa ndugu za marehemu kuja na kwenda kutambua mwili uliohifadhi wa katika chumba cha maiti ndani ya  hospitali ya wilaya Tarime  kwaajili ya maandalizi ya mazishi na wasiogope japo wamjue ndugu yao aliyekuwa jambazi hatari.

Kamanda Mwaibambe amemaliza kwa kutoa wito kwa wananchi wote wanaojuhusisha na matukio ya kihalifu kuacha mara moja kwani kila mara tunawakumbusha na kuwaasa kuwa mkono wa sheria ni mrefu tutakupata popoite ulipo mda wowote bila kujali wewe ni nani kwahali hiyo wajishugulishe na shuguli nyingine za kiuchumi zilizo halali.