Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imetoa msaada wa mashine mbili za kutunzia watoto njiti (Incubators) zenye thamani ya shilingi Milioni 25, kwa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga - Bombo, ikiwa ni moja ya mikakati ya kusaidia kupunguza vifo vya watoto njiti.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Abdi Makange amesema kuwa awali kulikuwa na mashine mbili tu pekee ambazo zilikuwa hazitoshelezi mahitaji, hivyo kuongezeka kwa mashine hizo mbili kutasaidia kuokoa maisha ya watoto hao ambao awali walikuwa wakipoteza maisha.

