https://monetag.com/?ref_id=TTIb Agizo la Rais Magufuli kwa Askari huyu baada ya kumkuta kituoni | Muungwana BLOG

Agizo la Rais Magufuli kwa Askari huyu baada ya kumkuta kituoni


Rais Magufuli ameagiza WP 4160 Beatrice Kayuni Mlanzi, kupandishwa cheo kutoka Koplo na kuwa Sajenti baada ya kuonesha utimilifu katika kazi.

Agizo hilo amelitoa jana Septemba 10, 2019, baada ya kupita katika kituo cha Polisi Selander Bridge.

Rais Magufuli alipita kituoni hapo akiwa njiani kurejea Ikulu, akitokea Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokwenda kumjulia hali Baba Askofu Mkuu Ruwa'ichi.

Rais alimjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi ambaye anapatiwa matibabu katika Taasisi hiyo ya MOI mara baada ya kufanyiwa upasuaji wa Kichwa.