Mwili wa Robert Mugabe umeondoka Singapore leo


Mwili wa rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe umeondoka Singapore mapema leo Jumatano asubuhi kwenda nchini Zimbabwe ambapo atazikwa baada ya maombolezo ya kitaifa.

Robert Gabriel Mugabe alifariki dunia Septemba 6 mwaka huu akiwa na umri wa miaka 95 nchini Singapore, ambapo alikuwa akihudumiwa kimatibabu kwa miezi zaidi ya mitano.

Rais huyo wa zamani wa Zimbabwe anatarajiwa kuzikwa Jumapili, Septemba 15 baada ya sherehe rasmi ambayo itafanyika Jumamosi. Hata hivyo familia ya Zimbabwe haijakubaliana na serikali sehemu ambapo atazikwa kiongozi huyo wa zamani wa Zimbabwe.

Tangu Ijumaa, Rais Emmerson Mnangagwa ametangaza maombolezo ya kitaifa na kumpa mtangulizi wake hadhi ya "shujaa wa kitaifa", ambayo inampa nafasi kuzikwa katika "makaburi ya Mashujaa wa Taifa". Lakini familia ya rais haijajapendelea kiongozi wao kuzikwa katika makaburi hayo.

Mishoni mwa wiki iliyopita mpwa wa Mugabe, Leo Mugabe alisema hajui ni wapi mjomba wake alitaka kuzikwa. Lakini mazishi katika makaburi ya Mashujaa wa Taifa, kama ilivyopangwa kabla ya kutimuliwa kwake madarakani.