Dondoo muhimu unayopaswa kuijua kuhusu maisha ya mafanikio

Kama ungetoa nafasi kwa watu kuchagua kati ya mafanikio na matatizo, wengi wangechagua mafanikio na kuachana kabisa na matatizo au changamoto katika maisha; kwa sababu licha ya kuwa sehemu ya maisha hakuna anaepokea matatizo kwa furaha.

Kama mafanikio na matatizo zingekua bidhaa ambazo watu wawili wamefungua biashara mmoja akiuza matatizo na mwingine akiuza mafanikio, hauhitaji kuwa mtabiri kujua kuwa katika kipindi cha muda mfupi mfanyabiashara anaeuza matatizo atakua amefilisika kabisa kwa kukosa wateja huku anaeuza mafanikio akijilimbikizia utajiri mkubwa katika kipindi cha muda mfupi.

Karibu tena msomaji wetu katika mtandao wetu wa maishanifursa. Leo tutajikita katika mada ambayo nimeipa kichwa “USITAFUTE KAZI TAFUTA MATATIZO” Nakushukuru sana kwa kuendelea kufuatilia kazi zetu uwepo wako ni muhimu sana kwa kazi yetu kwani bila wewe kazi yetu haina maana.

Ndio maana watu wengi wameingia katika mtego wa kudanganywa kupita njia ya mkato kufikia mafanikio ya haraka, baada ya kuonyeshwa dalili bandia kuwa wakifanya kitu fulani watafaniwa haraka;matokeo yake wamepoteza hata amali chache walizokua wanamiliki.

Maisha ni fursa mtambuka ambayo yenyewe imejaa fursa za kila aina, ikiwemo fursa yenye thamani kubwa iliyojificha nyuma ya matatizo au changamoto mbalimbali tunazokutana nazo katika maisha.

Kupitia makala hii fupi leo nataka tuangalie pamoja aina mbili za watu duniani ambao kila mmoja anamhitaji mwenzake kwa kiwango ambacho huwezi kuamini.

Inasemekana dunia ina watu karibu bilioni 8 kwa sasa hiyo ni fursa ambayo imewagawa watu katika makundi mawili muhimu, kundi moja kubwa ambalo linaongoza kwa wingi wa watu na kundi la pili ambalo linaongoza kwa nguvu ya maarifa.

Kundi moja kubwa la wakazi wa dunia ni lile la watu wenye matatizo katika maeneo mbalimbali ya maisha yao. Hawa wana matatizo ambayo ufumbuzi wake hawana na lingekua jambo la faraja kwao kama angetokea mtu ambaye ana njia au majibu ya changamoto au matatizo yao watakua tayari hata kumlipa mtu huyo kwa njia itakayoleta suluhu ya matatizo yao.

Kundi lingine ni kundi la watu adimu ambao wao wana maarifa na njia ya kujibu na kutatua changamoto na matatizo mbalimbali yanayokabili watu mahali popote duniani.

Kinachofanya watu katika makundi haya mawili muhimu kutofautiana sana ni namna wanavyoitazama dunia kwa macho ya ndani na maarifa waliyonayo kutafsiri ukweli halisi wa maisha.

Wakati kuna watu katika kundi moja wanaona kana kwamba dunia inataka kusimama wanapoingia kwenye matatizo, watu katika kundi la pili wanachukulia matatizo kama fursa maana wanatofautiana wanavyotazama mambo ndani na nje.

Kuna aina mbili za macho kwa kila mwanadamu ambayo amepewa,macho ya mwili (sight) na macho ya nafasi (mind) na hapo ndipo tofauti ya watu ilipo;japokua watu wengi huchanganya kwa kudhani tofauti iko kwenye sura zao.

Nenda ulaya, Marekani, Afrika, Asia n.k utashangaa kuona kuwa kila mahali kuna watu ambao wana matatizo na watu wanaoishi vizuri ni wale wanaokua sababu ya suluhu za changamoto na matatizo mbalimbali yanayowakabili watu. Mtu mwenye majibu ya matatizo ya watu hawezi kutafuta watu ila watu watamtafuta na kumlipa kulingana na huduma anayowapa.

Watu wengi wanahangaika kutafuta kazi itakayowasaidia kufikia mafanikio katika maisha yao na pengine kusaidia watu wengine kufanikiwa pia; lakini changamoto kubwa ni kwamba wanapishana na kanuni ya kufikia hayo mafanikio.

Mhubiri na mwalimu maarufu wa maswala ya dini na maisha hayati mchungaji Dr Myles Munroe katika moja ya mafundisho yake amesisitiza sana juu ya umuhimu wa matatizo katika maisha ya watu na jinsi ambavyo ana thamani kubwa mtu anaeleta majibu ya matatizo mbalimbali yanayokabili binadamu.

Watu wengi waliofanikiwa iwe kupitia biashara au huduma utagundua majukumu yao yanahusisha kwa namna moja kujibu matatizo ya watu kwa njia moja au nyingine.

Mafanikio ya mtu hayako katika kazi ya ajira alikoajiriwa au atakakoajiriwa mtu hiyo,ila yako katika uwezo na maarifa mtu huyo aliyo nayo kutatua changamoto na matatizo mbalimbali yanayokabili binadamu mahali popote alipo.

Kwa hiyo mtu akitaka kufanikiwa asitafute kazi ila atafute matatizo; na kumbuka matatizo yanakaa kwa watu kwa hiyo atafute watu wenye matatizo ili apate kuwasaidia kupata majibu ya changamoto na matatizo yao;kupitia karama na kipaji mtu huyo alichojaliwa na Mungu.

Kila binadamu ameumbwa akiwa na kitu cha pekee ndani mwake, kwa ajili ya kuifanya dunia kuwa mahali pazuri pa kuishi;yeye mwenyewe na binadamu wengine.

Watu wengi wanahaha kutafuta kazi usitafute kazi, tafuta matatizo uwasaidie watu kutatua matatizo yao kwa kutumia karama na kipaji chako.

Naamini utakuwa umepata kitu kupitia makala hii fupi. Ukiwa na uhitaji wowote au ushauri katika eneo lolote la kuboresha maisha,biashara yako au hata una wazo kuanzish kitu fulani lakini unakwama;usisite kuwasiliana nasi kupitia njia za mawasiliano hapo chini. Aidha kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno, whatsapp kupiga simu au kututumia barua pepe nasi tutarudi kwako mapema iwezekanavyo.Tutashukuru kama watakaotutafuta wakiwa ni wale ambao kweli wanamaanisha.