Mbinu zitakazokusaidia kujitibu tatizo la nguvu za kiume



Tatizo la nguvu za kiume limekuwa ni tatizo kubwa sana, tumekuwa tukishudia michepuko mingi ikiongezeka kila kukicha huku wengine wakithubutu hata kuvunja mahusiano yao hii ni kwa sababu ya tatizo hili, hivyo ili kuweza kuondokana na tatizo hili ipo haja ya kutambua namna ambavyo tunaweza kujitibu tatizo hilo

Zifuatazo Njia  za kujitibu tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume: 

Acha mawazo 
Mawazo na mfadhaiko huondoa mtiririko mzuri wa damu kwenda kwenye uume na kusababisha nguvu kupungua nguvu za kiume na hata uume wenyewe.I kiwa unasumbuliwa na mfadhaiko au stress uangalifu mkubwa unahitajika kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote.

Katika hali ya mfadhaiko wa akili utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi kwa mfano, wanandoa wanapaswa kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi, shida ni pale kama mke akili yake ni ndogo kwani badala ya kufunga na kuomba kwa Mungu huenda akaenda kukutangaza kwa majirani!.

Jitibu magonjwa yafuatayo 
Kama tatizo limesababishwa na magonjwa kama kisukari, vidonda vya tumbo, shinikizo la juu la damu au uzito kupita kiasi ni vema ukajitibu kwanza maradhi haya. Tatizo ni kuwa watu wameaminishwa kwamba maradhi haya hayana dawa jambo ambalo si kweli.

Kisukari, shinikizo la juu la damu, vidonda vya tumbo na hata uzito kupita kiasi ni magonjwa yanayotibika kabisa hasa kwa kutumia dawa mbadala na kufuata muongozo sahihi katika kula na kunywa kwa kipindi cha majuma kadhaa.

Acha vilevi 
Kama tatizo linatokana na matumizi ya vilevi, hatua ya kwanza ni kuviacha kwanza hivyo vilevi. Ndiyo kuviacha kwanza, unatakiwa ujiulize mwenyewe kipi ni mhimu kwako ndoa yako au hivyo vilevi? Mtu anayejali vilevi kuliko hata afya yake hafai.

Kuna watu wanajidanganya kwamba ukitumia sijuwi kilevi fulani nguvu zinaongezeka, ni kweli zitaongezeka hapo mwanzoni mwa matumizi ya hicho kilevi lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo utakavyoendelea kuwa mtegemezi wa hicho kilevi na itafika siku hata hicho kilevi hakitasaidia kitu na hapo ndipo hatari zaidi ya kutotibika tatizo lako itakapojitokeza.

Fanya mazoezi ya viungo 
Zingatia sana umhimu wa mazoezi ya viungo. Bila kujishughulisha na mazoezi ya viungo kila siku itakuwa ni vigumu sana kwako kupona tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Kutengeneza mishipa na kupunguza uzito isiwe ndiyo sababu pekee ya kwenda gym. Kama unahitaji nguvu za kiume na uume wenye afya, unahitaji kujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara ili kusafisha mishipa ya damu na hivyo kuongeza kiasi cha utiririkaji wa damu kwenda kwenye uume.

Kama uzito wako upo juu sana na ni mnene fanya mazoezi ya kukimbia (jogging) kila siku kwa mwezi mmoja mpaka miwili. Kama uzito wako upo sahihi tu kwa mjibu wa urefu wako fanya sana mazoezi ya kuchuchumaa na kusimama. Una chuchumaa na kusimama mara 25 mpaka 30, unaweza kupumzika dakika mbili unaendelea tena kuchuchumaa na kusimama hivyo hivyo unapumzika dakika 2 mpaka mizunguko (rounds) mitano kila siku.

Tumia kitunguu swaumu 
Chukuwa punje 6  za kitunguu swaumu, menya na uzikate vipande vidogo vidogo kisha meza na maji vikombe 2 kutwa mara 1 kwa mwezi mmoja.

Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida nyingi mwilini ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na sifa zifuatazo:

Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.

Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na hivyo kupunguza madhara ya kisukari.

Ukivikata vipande vidogo vidogo hivi (chop), vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo kwa kitaalamu kama ‘Allicin’ ambayo ni dawa dhidi ya bakteria, na ‘Phytoncide’ ambayo huua fangasi mbalimbali mwilini.

Kula tikiti maji 
Tunda hili lina faida nyingi pamoja na kuwa ni chanzo kikuu cha Protini, Mafuta, Nyuzinyuzi, Wanga,Calcium, Phosphorus, Chuma,Vitamin A,B6,C. Potasium, Magnesium, Carotene, anthocyanins na Virutubisho vingine vingi.

Tunda linasaidia kuwa na uwezo mkubwa wa kuimalika kwa misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri na kuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la juu la damu.

Kula tikiti maji kila siku huku ukitafuna na zile mbegu zake, fanya mara hivi mara kwa mara.

Kula ugali wa dona 
Kula ugali wa dona kila siku. Ni mhimu kuachana na mazoea ya kula ugali wa sembe. Ugali wa dona una virutubisho vingi na mhimu kwa ajili ya afya ya mwanaume. Kama ugali wa dona unakukera jaribu kufanya hivi, chukuwa mahindi kilo 10 ongeza ngano kilo 3 na usage kwa pamoja, ugali wake huwa ni mlaini, mzuri na mtamu na unaweza kula na mboga yoyote tofauti na lile dona la mahindi peke yake. Fanya hivi katika familia yako kwa maisha yako yote.

Kunywa maji mengi kila siku 
Kunywa maji ya kutosha kila siku bila kusubiri kiu. Kila mtu anahitaji glasi 8 mpaka 10 za maji kila siku. Maji ni mhimu katika kuongeza damu, kusafisha mwili na kuondoa sumu mwilini.