Rais wa Zambia ahuzunishwa na ajali mbaya ya Barabarani


Rais wa Zambia Edgar Lungu siku ya jana aliomboleza vifo vya watu sita waliofariki katika ajali ya barabarani katika wilaya ya Chingola katika mkoa wa Copperbelt.

Ajali hiyo ilitokea Jumapili wakati gari walilokuwa wakisafiria lililongana na lori na kusababisha vifo vya watu sita na kujeruhi wengine 26.

Katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake, Lungu alionyesha kusikitishwa na ajali hiyo mbaya na aliwataka Wakala wa Uchukuzi na Usalama Barabarani (RTSA) mara kwa mara kuangalia barabarani ili kuondoa magari yaliyoharibikia barabarani ambayo yanahatarisha madereva.

"Inasikitisha kwamba watu waliangamia kwa sababu lori liliachwa barabarani kwa muda mrefu. RTSA na polisi lazima wawe waangalifu ili kupunguza ajali za barabarani," alisema.