Kocha Hemedi Moroko atangaza kikosi cha Zanzibar Heroes


Na Thabit Madai, Zanzibar

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar herous) Hemed Suleimani Moroko ametangaza kikosi cha wachezaji 50 ambao wanatarajia kuingia kambini kujiandaa na Mashindano ya Cecafa Seniors Challenge Cup yanayotarajiwa kuanza mwezi ujao Nchini Uganda.

Akitangaza kikosi hicho leo katika ukumbi wa shirikisho la soko visiwani Humo ZFF ,Kocha Moroko alisema kikosi hicho cha wachezaji 50 kimejumuisha wachezaji wa  ligi kuu Zanzibar na wa ligi kuu Tanzania bara.

Alisema kuwa kigezo kikubwa ambacho ameangaliwa katika kuchagua wachezaji hao ni kuwapa nafasi wachezaji ambao wanauwezo na hawaonekani katika timu zao.

“Kikosi hichi kimesheheni wachezaji ambao wanauhodari lakini wamekuwa hawaonekani katika vilabu ambavyo wanachezea” alisema Kocha Moroko.

Wachezaji hao ni

MAKIPA
1.Abdul-latif Said Masoud (Jamhuri)
2. Mohamed Abrahman (JKT TZ)
3.Mohamed Muali (Polisi Tz)
4.Abdallah Rashid "Babu" (Ruvu Shooting)
5.Haji Juma "Chafu" (JKU)
6.Ahmed Ali "Salula" (Malindi).

 WALINZI
1.Suleiman Said Juma (Zimamoto)
2.Mohammed Othman Mmanga (Polisi Tz)
3.Ibrahim Mohamed "Sangula" (KVZ)
4.Mwinyi Haji Ngwali (KMKM)
5.Juma Kukuti Adam (Polisi Tz)
6.Ally Haji (Mwenge)
7.Abdul Malik Adam (Mafunzo)
8.Ali Juma Maarifa (Malindi)
9.Issa Haidar Dau (JKU)
10.Abdallah Kheir (Azam)
11.Ibrahim Ame Mohd (Coastal Union)
12.Ally Ally (Yanga)
13.Abubakar Ali (Mlandege)
14.Ibrahim Hamad (Malindi)
15.Agrey Morris (Azam)
16.Abubakar Ame "Luiz" (Malindi).

 VIUNGO
1.Abdul aziz Makame (Yanga)
2.Abdul swamad Kassim (Kagera)
3.Awesu Awesu (Kagera)
4.Mudathir Yahya (Azam)
5.Is haka Said (KMKM)
6.Adam Ibrahim "Edo" (KMKM)
7.Kassim Suleiman (Azam)
8.Haroun Abdallah (Zimamoto)
9.Feisal Salum (Yanga)
10.Mohamed Issa (Yanga)
11.Mustafa Muhsin (Zimamoto)
12.Helefin Salum (Mlandege)
13.Baraka Shaaban (Ruvu Shooting)
14.Khalid Shaaban (Rich boys)
15.Abdallah Hassan Nassor (Polisi Tz)
16.Mohd Mussa (Mbeya City)
17.Mohamed Abdallah (Mlandege)
18.Ally Juma "Larson" (Mafunzo).

 WASHAMBULIAJI
1.Ibrahim Hamad "Hilika" (Zimamoto)
2.Abdul nassir Asaa (Mlandege)
3.Khamis Mussa "Rais" (Malindi)
4.Said Salum "Etoo" (Kipanga)
5.Ibrahim Abdallah (Malindi)
6.Mussa Ali Mbarouk (KMKM)

Alifafanua kuwa wachezaji hao wanatarajiwa kuanza ratiba ya mazoezi ya Asubuhi na Jioni kuanzia tarehe 14 mwezi huu.

“Tunaanza mazoezi na wachezaji ambao wanacheza Ligii kuu soka Zanzibar na baadae watajiunga wenzao ambao wapo nje ya Zanzibar” alifafanua Kocha Moroko.

Mara ya mwisho kufanyika Mashindano hayo ilikuwa mwaka 2017 Machakos nchini Kenya ambapo Heroes walipata nafasi ya pili baada ya kukubali kufungwa na wenyeji wao Kenya.
Mpya zaidi Nzee zaidi