Tambua biashara yenye mafanikio


Tambua kuwa kuna sifa za Biashara zinazoweza kumuweka mfanyabiashara kwenye mafanikio. Kwenye Biashara kuna sifa  ambazo huonekana zikimshawishi mfanyabiashara kuwa na ujasili wa kuendelea kufanya kazi yake na kupata faida zaidi , leo ningependa kuzungumzia sifa hizo.

Inawateja wengi.
Hii hutokana na mfanyabiashara anavyoweza kuwa karibu na wateja wake na kuwaelezea kuhusiana na bidhaa zake na jinsi ya kuzitumia pale wateja wake wanapo kuwa wanaitaji maelekezo kuhusu bidhaa hizo nakuhakikisha anamshawishi mteja mwenye hasira afurahi na aridhike na bidhaa hizo . Na ningependa uelewe kuwa biashara huwa inahitaji umakini wa hali ya juu ili mteja anapo kuwa na shida iwelahisi kumuelimisha na mteja kuondoka amelidhika na bidhaa yako.

Huwa na faida 
Faidi hiyo hupatikana pale unapokuwa unabuni mbinu mbadala ya kuhamasisha wateja wako waweze kukuelewa zaidi na kuendelea kuamini bidhaa yako. Mbinu unazo weza kubuni ni zipi, nikuhakikisha unaongeza kile kitu ambacho ni tofauti na cha washindani wako kitika biashara yani kubadili muonekano wako uwe wa hali ya juu zaidi kuliko wa washindani wako. Na ni muhimu utoe huduma nzuri zaidi kuliko ile inayotolewa na washindani wako. 

Ni ya kudumu.
Unapokuwa  unaboresha biashara yako na kuendelea kuithamini na kuhamasisha wateja wako waendelee kununua kwako ndipo  unapo fahamika zaidi. Pia huduma inakuwezesha kuuza kwa bei ya juu kuliko wengine na kuwezesha Biashara yako kudumu zaidi bila kupoteza wateja wako. Sasa basi thamini kazi yako iweze kudumu zaidi na kukuwezesha wewe kujipatia  kipato cha juu, sifa hizo ukizi fuata natumaini unaweza kufahamika zaidi na Biashara yako kudumu zaidi.