Afisa Madini aonya wachimbaji wadogo kuihujumu Serikali



Na Paschal Malulu-Kahama.

AFisa Madini Mkazi Mkoa wa Shinyanga Eng. Joseph Kumburu amewaonya Wachimbaji wadogo wa Madini ya Dhahabu katika Mgodi wa Kalemala Gold Rush ulipo katika kijiji cha Buswangili kata ya Bulyanuhulu,Halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga, kwa kitendo cha Kuikosesha mapato serikali.

 Aidha Afisa huyo Kumbulu alisema kuwa amekuwa akipata  malalamiko kwa baadhi ya wachimbaji wa Mgodi huo  kunyanyaswa na uongozi wa Rush hiyo huku ikiwatoza kiasi cha shilingi 150,000 kinyume na utaratibu pamoja na kuwatoza tozo mbalimbali zizizotamburika na Serikali.

 Alisema kuwa anataarifa zote juu ya ukwepaji kodi na na kuongeza kuwa licha ya shilingi 150,000 wanazotozwa Wachimbaji kwakila Duara kwa adhabu ya kuhama kwa wachimbaji na kurudi katika eneo lao wakitokea Namba Tisa kakola yalikofumoka Machimbo mengine pia Wachimbaji hao wanatozwa shilingi 1,000 na watu wawili tofauti kwa maana ya halmashauri na mmoja wa viongozi wa mgodi getini.

 Kufuatia hali hiyo Eng.Kumburu aliagiza mamlaka ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU Wilaya ya Kahama kufika katika Mgodi huo ili kuchunguza uhalali wa fedha zinazotozwa na viongozi wa mgodi huo na baadaye ichukue hatua kali kulingana na kuhujumu wachimbaji na wananchi kwa ujumla.

Mmoja wa wachimbaji hao Nyang’anyi Mwita akitoa malalamiko hayo mbele ya Afisa madini huyo kwa niaba ya Wachimbaji wenzake alisema kuwa, awali walikuwa wakichimba Madini ya Dhahabu katika mgodi huo na baada ya kupata taarifa ya kuvumbuka kwa Madini hayo katika eneo la Namba Tisa walikwenda huko  lakini waliporejea tena  katika eneo lao la kazi, uongozi wa mgodi huo wa Kalemela gold Rush ili wachimbe tena uliwapiga faaini ya kuanzia shilingi 150,000 ambazo walilipa bila ujanja.

“Awali tulikuwa tukichimba madini katika eneo hili,lakini baada ya kupata taarifa ya uwepo wa madini ya kutosha katika mgodi wa namba tisa tulielekea wote huko kuendelea na shuguli zetu za uchimbaji wa amdini”Alisema Mwita.

Aliongeza kuwa”Tuliporejea katika maduara yetu katika mgodi huu wa Kalemela Gold Rush tunashangaa kuona uongozi wa mgodi ukitutoza faini ya shilingi 150,000 kila duara kwa madai yakwamba tuliwakimbia na kuelekea kwenye mgodi mwingine .

Mwita aliendelea kumweleza Ofisa madini kuwa”Wachimbaji wote tulikubaliana kuwalipa kiasi hicho cha fedha na baadae tuliondoka kutafuta wafanyakazi wa mashimo hayo chakushangaza tuliporudi na wafanyakzi wetu tulielezwa  maduara yetu yameuzwa na wanachama wa kikundi cha Mgodi ikabidi tukimbilie ofisi za Madini Kahama kuomba Msaada maana tumeibiwa warejeshe fedha zetu,” alisema.

Hata hivyo Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji wadogo Wilayani Kahama(SHIREMA) Nicodemus Majabe alisema kuwa,serikali inafahamu kila kitu kinachoendelea katika mgodi huo,nakuwataka kuacha mchezo wa kucheza na Dhahabu kama ilivyo kwenye madawa ya kulevya na badala yake  kila mchimbaji apate haki yake ikiwa ni pamoja na kuweka wazi mambo yao.