Kama umeshindwa kufanya vyema katika jambo fulani jifunze kitu hapa

Unapofanikiwa na kung'ara wapo watu watakufurahia na kusherehekea nawe hata usio wajua.Na wakati huo huo wapo watu wataumia na kuomboleza kwa maumivu kwa nini umefanikiwa?kwa nini umeng'ara?tena unaowajua na usiowajua,wakaribu na wambali.

Na hata utakapoanguka na kufulia/kupigika kiuchumi,kimahusiano,kikazi, wapo watakao lia na kuumia na wewe.Na wakati huo huo kuna watu watashangilia hata usiowajua na kufurahia anguko lako huku wakisema afadhali yamemkuta akome kabisaa.
Ujue kuna watu hupenda kuona mtu amepitia maumivu flani wao inawapa raha sana.

Maana yake nini .....maisha yako yapo mikononi mwako.Kwa raha au furaha,majonzi na huzuni,kushindwa au kushinda vyote vipo mikononi mwako.

Paka ni mnyama mwenye kitu cha pekee sana.Paka huwa haanguki puuu kama kiroba.

Anaanguka huku akiwa anajua anaanguka na akilini anajiandaa kabla hajafika chini kudondoka tayari huanza kusimama kabla ya kufika chini.Na akifika chini anatua kwa miguu yake minne tayari kuendelea na safari kama hakuna kilichotokea.

Kibinaadamu huwezi kuwa kama paka ila unaweza kujaribu vitu kadhaa.Unapoanguka usikae muda mrefu katika anguko tafuta suluhisho.Acha kukaa hapo unajihurumia. Anza upya,Badili uelekeo,Badili mbinu na formula fanya iwezekanavyo..na usiwawaze watu wala kuwafikiria maana wakati huo wapo wanaofanya party kufurahia anguko lako na wapo wanaoumia na wewe.