Loading...

1/16/2020

Waziri Ndalichako azindua shule ya Mrisho Gambo

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, ameweka Jiwe la Msingi katika Shule ya Sekondari MRISHO GAMBO, iliyoko katika Kata ya Olasiti jijini Arusha.

Shule hii ndiyo Shule ya kwanza ya Kisasa itakayokuwa ikiendeshwa kwa mfumo wa Kisayansi (STEM) yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati.

Waziri Ndalichako, amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha pamoja na Wadau mbalimbali wa maendeleo Mkoani humo, kufanikisha ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kisasa MRISHO GAMBO.

Prof. Ndalichako amesema katika kutambua juhudi hizo, serikali itawezesha Ujenzi wa Mabweni mawili pamoja na kufanya mchakato wa kuipandisha hadhi kuwa Shule ya Upili.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger