CAF: Viwanja vya mpira Zimbabawe havitimizi viwango kuchezwa mechi za kimataifa


Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetangaza jana kwamba viwanja vya Zimbabwe havitimizi viwango vinavyoruhusu kuchezwa mechi za kimataifa.

Tangazo hilo ni pigo kubwa dhidi ya juhudi za Zimbabawe za kutaka kutambuliwa kimataifa. Jumuiya ya mpira wa miguu ya Zimbabwe ZIFA imesema walipokea barua hiyo na walifadhaika.

Zimbabwe italazimika kutafuta kiwanja mbadala cha kucheza mechi ijayo dhidi ya Algeria.

 Msemaji wa jumuiya hiyo, ZIFA Xolisani Gwesela amesema watalazimika kama taifa kushirikiana ili kutimiza viwango vinavyohitajika.
Mpya zaidi Nzee zaidi