Tunda la bibo kuwa fursa mpya kwa wakulima

Na Hamisi Abdulrahmani, Mtwara.

  TAASISI ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Naliendele Mtwara(TARI) imesema kuwa tunda la bibo linaweza kuwa fursa mpya kwa wakulima wa zao la korosho kujiinua kiuchumi kwa kuchakatwa na kutengeneza mvinyo na hiyo itaondoa dhana ya kutegemea mbegu(KOROSHO) pakee yake.

 Kauli hiyo ilitotolewa jana mkoani Mtwara na kaimu mkurugenzi wa Taasisi hiyo,Dkt.Fortunus  Kapinga alipokuwa akizungumza wakati wa kikao cha baraza la biashara mkoa wa Mtwara kilichofanyika mkoani hapa.

  Alisema kwa muda mrefu sasa taasisi hiyo imekuwa ikifanya utafiti wa zao la korosho na hatimaye utafiti uligundua bidhaa mbalimbali ikiwemo mvinyo wa mabibo kuwa ni bora na unathamani kubwa katika soko

   Dkt.alisema kutokana na ugunduzi huo mpya unaotokana na bibo la zao la korosho kuweza kutengeneza mvinyo hivyo utafiti huo utamuwezesha mkulima kunufaika na mazao mengine ya korosho kuliko ilivyo hivi sasa ambapo thamani ya korosho imeonekana kwenye mbegu yake pekee.

   Alisema kuwa kwa ugunduzi huo utaongeza uzalishaji na usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi na hivyo kuiongezea serikali mapato na kwamba hata wakulima pia wataweza kujiinua kuchumi kupitia zao la korosho.

  Dkt.Kapinga alisema teknolojia hiyo ya utengenezaji wa mvinyo kwa kutumia mabibo ya zao la korosho ambapo teknolojia hiyo itakuwa ya kwanza hapa nchini na kwamba hiyo inajibu hoja ya muda mrefu ya uongezaji wa thamani ya zao la korosho kwa kutumia bidhaa  zingine zinazotokana na zao hilo.

 “Nisema wazi kuwa teknolojia hii itakuwa ya kwanza hapa nchini na kwa muda mrefu sasa hatua hii itakuwa ikijibu ile hoja ya uongezaji thamani ya zao la korosho kwa wakulima kwa kutumia bidhaa nyingine zinazotokana zao hili,”alisema Dkt. Kapinga

   Alisema kwa sasa wakulima hawana sababu ya kuhofia utunzaji na usafirishaji wa mabibo kwani mabibo yaliyofanyiwa utafiti na kubainika kuwa na sifa ya utengenezwaji wa mvinyo ni yale yaliyokaushwa.

   Dkt.Kapinga aliongeza kuwa mazao mengine ya korosho yaliyofanyiwa utafiti na taasisi hiyo ni pamoja na nishati na mafuta ya kuulia wadudu ambayo yanatengenezwa kutokana na maganda ya korosho,maziwa yanayotengenezwa kutokana na mbegu za korosho na pia siagi ya korosho.

  Naye mkuu wa mkoa wa Mtwara,Gelasius Byakanwa alisema serikali mkoani humo inapongeza hatua hiyo,  kwa sababu itaongeza thamani ya zao la korosho lakini hata uchumi wa mkulima mmoja mmoja utafunguka zaidi.

  Alisema anawataka wananchi wa mkoa  huo kumchangia fursa hiyo adimu na kwamba anawataka wafanyabishara wa ndani wanaoshughulika na biashara ya korosho kuanzisha mashamba ili kuongeza uzalishaji, kwa vile serikali iko bega kwa bega kuhakikisha wanafainikiwa fursa hiyo.
Mpya zaidi Nzee zaidi