China kuwapeleka mabata Pakistan kukabiliana na nzige


China inapanga kupeleka takriban mabata elfu 100 kuisaidia Pakistan kukabiliana na idadi kubwa ya nzige waliovamia taifa hilo.

Haya ni kwa mujibu wa gazeti la Ningbo Evening lililoripoti hayo hii leo. Gazeti hilo limeendelea kuripoti kuwa mabata hao watapelekwa kutoka mkoa wa Mashariki wa Zhejiang kufuatia kutangulia kwa kundi la wataalamu wa China nchini Pakistan kushauri kuhusu jinsi ya kukabiliana na nzige hao waliovamia nchi hiyo katika kile kinachotajwa kuwa uvamizi mbaya zaidi katika muda wa miaka 20.Kwa mujibu Lu Lizhi, mtafiti katika taasisi ya teknologia ya kilimo mkoani Zhejiang, miongo miwili iliyopita,

China iliwapeleka mabata hao ambao lishe yao asilia inajumuisha wadudu kukabiliana na uvamizi kama huo wa nzige katika eneo la Xianjiag Kaskazini Magharibi mwa nchi hatua iliyotajwa kupata ufanisi.

Pakistan ilivamiwa na kundi la nzige mwaka jana ambalo lilivamia mmea wa pamba na sasa ni tatizo kwa kilimo cha ngano.
Mpya zaidi Nzee zaidi