Pais wa Russia, Vladimir Putin leo ameanika mpango wa siri wa kumtumia mtu anayefanana naye kujitokeza hadharani badala yake, huku akisisitiza kuwa aliupinga mpango huo na kwamba yeye ndiye Putin halisi.
Kauli ya Putin imeonyesha dhana iliyoenea katika mitandao ya kijamii kwamba kwa miaka kadhaa kiongozi huyo wa Russia amekuwa akiwakilishwa na mtu anayefanana naye, haikuibuka bila ya kuwepo na misingi.
Shirika la habari la serikali la TASS lilimuonyesha Putin orodha ya misako inayofanywa katika mtandao wa internet unaotumia lugha ya Russia, ukiwemo ule wa "Putin double proof (uthibitisho wa pacha wa Putin)". "Ni wewe halisi?" mmoja aliuliza. "Ndio," alisema Putin.
Rais huyo alisema hajawahi kuwa na mtu anayefanana naye, lakini alipoulizwa kama wazo hilo liliwahi kujadiliwa, alithibitisha kuwa liliwahi kujadiliwa.
"Nilikataa kuwa na mtu wa pili," alisema Putin. "Ilikuwa ni wakati mgumu kuliko wote wa vita dhidi ya ugaidi."
Putin akiwa waziri mkuu na baadaye rais alisimamia vita ya pili dhidi ya watu waliokuwa wakitaka kujitenga wa Chechnya kuanzia mwaka 1999 hadi 2000.
Baada ya majeshi ya Russia kujitangaza washindi, mashambulizi ya kigaidi yakaanza Caucacus Kaskazini wakati milipuko ya mabomu yaliyokuwa yanabebwa na watu wanaojitoa mhanga, ikapataa katika miji mikubwa.
"Hiyo ilikuwa mapema miaka ya 2000?" aliuliza Andrei Vandenko, ambaye anafanya mfululizo wa mahojiano na Putin katika kuadhimisha miaka 20 tangu awe rais.
"Ndio," alisema Putin.
"Mtu nayefanana naye angekuwa akienda sehemu ambazo mambo hayakuwa mazuri?" aliuliza Vandenko.
"Ndio, nenda, hadharani," alithibitisha Putin. Mwaka 2015, Putin hakuonekana hadharani kwa siku 10, na kusababisha ubashiri kuwa amepata mtoto mwingine, amekamatwa, ameugua amefanyiwa upasuaji kumbadili sura au hata amefariki.
"Inakera kama hakuna minong'ono," alisema Putin baada ya kuonekana tena hadharani.
