Maafisa wa matibabu nchini Ujerumani, leo wamechukua hatua ya kukabiliana na mripuko wa virusi vya corona nchini humo huku idadi ya visa vya maambukizi ikiongezeka kwa kasi na viwanda vikionya kuhusu athari kubwa kwa uchumi.
Mamia ya watu walijiweka chini ya karantini katika nyumba zao katika jimbo la Magharibi la North Rhine Westphalia baada ya mwalimu wa chekechea aliyekuwa amehudhuria sherehe za kanivali kuthibitishwa kuambukizwa virusi hivyo.
Takriban visa 10 vipya vimethibitishwa kote nchini Ujerumani na shughuli ya kuwatafuta watu wengine walioambukizwa iliendelea hii leo, hii ikiwa ni kwa mujibu wa waziri wa afya wa Ujerumani Jens Spahn amesema kuwa Ujerumani iko mwanzoni mwa janga la virusi vya Corona na kwamba visa vipya huko North Rhine-Westphalia na Baden-Württemberg ni ishara ya hali hiyo.Jens ameongeza kuwa ni vigumu kufuatilia mnyororo wa maambukizi ya virusi vya Corona.